Kocha wa
zamani wa Yanga, Hans van Pluijm amesema siku moja atarejea jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
kutoka Accra, Ghana, Pluijm amesema amekumbuka maisha ya jiji la Dar es Salaam
na rafiki zake kibao.
“Ndani ya
muda mfupi nilikuwa na rafiki wengi na Dar nilikuwa nimeizoea sana.
“Nililazimika
kuondoka kwa kuwa ni kazi, lakini nimepakumbuka sana.
“Siku moja
ninaweza kurudi tena, sijajua kama ni kuja kufanya kazi au kuwasajilia rafiki
zangu,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi.
Pluijm
aliinoa Yanga kwa nusu msimu kabla ya kuamua kuondoka kwenda Saudi Arabia
ambako amepata mkataba mnono.
Baada ya kuchukua nafasi ya Ernie Brandts katikati ya msimu, Pluijm aliingoza Yanga kushika nafasi ya pili baada ya mabingwa wapya Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment