Timu mbili
za nchini DR Congo moja ikiwa ni DC Motemba Pembe zimeendelea kusubiri kwa hamu
ili zipate nafasi ya kumtwaa mshambuliaji, Amissi Tambwe.
Timu hizo
mbili zipo tayari kumwaga mamilioni ili kumpata mshambuliaji huyo, mmoja wa
wakali kabisa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Tambwe raia
wa Burundi amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Msimbazi na habari za uhakika
kutoka ndani ya Simba, zimeeleza timu hizo za DR Congo zinamtaka Tambwe baada
ya kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.
“Lakini
Simba hawajasema kitu na Wakongo wanasubiri kwa hamu, uongozi ukitoa jibu kuwa
unataka shilingi ngapi, kila kitu kitakuwa wazi,” mtoa taarifa alisema.
Tambwe
ambaye yuko jijini Dar es Salaam, pia alisema timu hizo ziliwahi kumtafuta naye
akazikabidhi kwa Simba.
“Bado nina
mkataba wa mwaka mmoja, hivyo nilifuata utaratibu,” alisema Tambwe na kuongeza:
”nikawaambia wawasiliane na Simba, wameniambia wamefanya hivyo na sijui
kinachoendelea hadi sasa.”
0 COMMENTS:
Post a Comment