Wala hauhitaji kuambiwa kuhusiana na anayepania
au kutaka kufanya vema katika kazi yake, angalia matendo yake.
Kipa wa mpya wa Simba, Mohamed Shariff amekuwa
akifanya mazoezi kwa nguvu sana.
Shariff maarufu kama Casillas ameungana na Simba
akitokea Mtibwa Sugar na amekuwa anaonekana ana kazi ya kuwania namba kutoka
kwa Ivo Mapunda.
Hata hivyo kipa huyo bora wa Ligi Kuu Bara msimu
uliopita, anaonekana ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi.
Katika mazoezi ya siku mbili ya Simba ameonyesha
nia kwamba anataka kufanya kitu na hakusubiri kuhimizwa, badala yake alikuwa
kati ya wachezaji waliofanya mazoezi kwa kiwango sahihi alichotaka kocha
Selemani Matola.
0 COMMENTS:
Post a Comment