Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,
Zacharia Hans Poppe ndiye anasubiriwa ili kumaliza suala la mkataba wa Kocha
Zdravko Logarusic.
Loga alianza majadiliano na Hans Poppe mara
tu baada ya mwisho wa msimu uliopita.
“Hivyo tunalazimika kumsubiri mwenyekiti wa
kamati ya usajili ili kumaliza zoezi hilo,” alisema Said
Tully ambaye ni mmoja
wa wajumbe wa kamati ya usajili.
“Akiwepo Hans Poppe na sote pamoja, itakuwa
lahisi kujua walianza vipi, walifikia wapi na itakuwa lahisi kulijadili na
kulimaliza.
“Hivyo kwa pamoja tutavuta subira kidogo na
kumsubiri Hans Poppe, atakapokuja basi tutalifanyia kazi suala hilo ili lifikie
mwafaka,” alisema Tully.
Loga bado hajasaini mkataba mpya na zoezi
hilo huenda likakamilika baada ya siku mbili atakapokuwa amerejea mwenyekiti
huyo.
Kocha huyo Mcroatia aliifundisha Simba kwa
nusu msimu na baadaye akarejea kwao Croatia kwa mapumziko.








0 COMMENTS:
Post a Comment