Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kamati yake ya
usajili umeanza kazi ya kusaka viungo wawili na mshambuliaji mmoja ili ifunge
usajili.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza,
kamati ya usajili imeanza zoezi hilo ikiendelea kuitumia ripoti ya kocha huyo.
“Kazi imeanza haraka na ndani ya siku chache tutakuwa
tumewapata viungo hao, lengo ni kukamilisha ripoti ya kocha,” kilieleza chanzo.
Tayari Simba imefanya usajili wa zaidi ya wachezaji
watatu kwa lengo la kujiimarisha na moja ya pendekezo la Logarusic ilikuwa ni
nafasi ya kipa na Simba imemsajili Hussein Sharrif ‘Cassilas’.








0 COMMENTS:
Post a Comment