July 18, 2014



Mama mzazi wa Cristiano Ronaldo amejikuta akimwaga machozi wakati akielezea namna alivyotaka kuitoa mimba ya mwanaye huyo ambaye ni staaa.
 
Dolores Aveiro ameyasema hayo nchini Ureno wakati akizindua kitabu chake na kuhadithia kwamba daktari ndiye alikataa kuitoa mimba ya Ronaldo.
Kutokana na daktari kukataa, Dolores alirudi nyumbani na kunywa bia ya moto halafu akafanya mazoezi makali na lengo lilikuwa ni kuona mimba hiyo inatoka.

“Lakini siku moja Ronaldo alijua kuhusiana na hilo, akanieleza maneno yaliyoniuma sana, kwamba nilitaka kuitoa mimba yake lakini yeye ndiye rafiki na msaada kwangu,” alisema Dolores.

Ronaldo anayekipiga Real Madrid ana kaka yake pamoja na dada wawili na wamekuwa wakiishi kwa umoja na ushirikiano wa karibu sana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic