Mchezaji Abdallah Ugwadu wa timu ya Mazombi
FC ya Buguruni, alijikuta akianguka uwanjani na kuzimia kwenye mchezo
uliozikutanisha timu hiyo dhidi ya Wavuja Jasho ya Magomeni, uliopigwa kwenye
Uwanja wa Malala, Magomeni.
Championi
Jumamosi, lililokuwepo uwanjani hapo liloshuhudia
tukio hilo na kumfuata Ugwadu ambaye alipata fahamu baada ya kutolewa nje ya
uwanja na kuzungumza naye ambapo alisema tukio hilo lilitokana na kufunga mwezi
wa Ramadhan, ambapo alicheza mechi hiyo akiwa amechoka sana kutokana na swaumu.
SOURCE: CHAMPIONI JUMAMOSI







0 COMMENTS:
Post a Comment