Uongozi wa
timu ya Mbeya City ya Mkoani Mbeya, imesogeza mbele tarehe ya kuanza mazoezi
kufuatia kusogezwa mbele kwa ligi kuu.
Awali timu
hiyo ilikuwa iingie kambini Julai 19 tayari kwa kuanza maandalizi ya msimu ujao
wa ligi kuu lakini wameamua kubadilisha kufuatia kusogezwa mbele kwa ligi hiyo
ambayo sasa itaanza Septemba 20.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emannuel Kimbe ameeleza kuwa
kikosi chao kinatarajia kuingia kambini Agosti 15 kwa ajili ya kuanza
maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
“Tumeamua
kusogeza mbele tarehe ya kungia kambini kufuatia TFF kusogeza mbele ligi, hivyo
tunatarajia kuingia kambini Agosti 15 au 16 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya
msimu mpya.
“Kuhusu
mechi za kirafiki kocha ndiye atakayeamua anahitaji ngapi na sisi kama uongozi
tutafanya utekelezaji kufuatia maombi yake,” alisema Kimbe.








0 COMMENTS:
Post a Comment