July 15, 2014

MAGORI AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA YANGA.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Taifa (NSSF), Crescentius Magori amewapa daraja la kutosha wachezaji wa Yanga.

Magori ambaye ni mjumbe wa kamati ya usajili ya Simba alitoa darasa hilo leo akiwaelezea wachezaji wa Yanga umuhimu wa kukopa nyumba bora za NSSF.

Pamoja na wachezaji hao, Magori alitoa darasa kwa Kocha Mkuu Marcio Maximo pamoja na wasaidizi wake.
Wachezaji hao walipata nafasi ya kumuuliza maswali bosi huyo wa NSSF ambaye aliyajibu kiutaalamu hadi wote waliporidhika.
Wachezaji wa Yanga wanaruhusiwa kukopa nyumba katika maeneo ya Kijichi na Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Yanga inakuwa klabu ya kwanza nchini kuwafanyia wachezaji wake na staff wa benchi la ufundi mpango huo mzuri unaojali maisha yao ya sasa na baadaye.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic