July 17, 2014



Beki Rio Ferdinand amesaini kuichezea Queen Park Rangers ambayo imerejea Ligi Kuu England.

Timu hiyo maarufu kama QPR kutoka Loftus Road imekamilisha usajili huo na kumnasa mkongwe huyo wa zamani wa Man United.
Rio atalamba mkataba wa miezi 12 tu, yaani mwaka na atakuwa akichukua kitita cha pauni 70,000 kwa wiki.
Awali Rio alionekana kutaka kubaki Man United na kucheza kwa msimu mmoja zaidi, lakini akatolewa nje.
Wengi hawakuamini angeondolewa katika hatua za mwisho na baadaye alilaani na kudai ilichangia kwa kuwa asili yake ni Peckham, London na si kijana wa Manchester kama ilivyo kwa akina Paul Scholes, Ryan Giggs na wengine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic