KIONGERA AKIITUMIKIA KENYA KATIKA MECHI DHIDI YA MISRI. |
Kamati ya usajili ya Simba
imeamua kuachana na mshambuliaji Modo Kiongera anayekipiga KCB na timu ya taifa
ya Kenya, Harambee Stars.
Uamuzi huo unatokana na
Simba kukasirishwa na kitendo cha Kiongera kuongeza bei ya usajili katika hatua
za mwisho, tofauti na walivyokubaliana awali.
Habari za uhakika kutoka
ndani ya Simba zimeeleza, Kiongera alibadilika na kutaka fedha nyingi zaidi ya
zile walizokubaliana na Simba.
“Kweli kama imeamua kuachana
naye, maana awali makubaliano yalikuwa achukue kiasi fulani na akakubali kuja
Dar, lakini mwishoni ameamua kubadilika na anataka zaidi,” kilieleza chanzo.
Kiongera alikuwa kati ya
chaguo la Kocha Zdravko Logarusic ambaye alimtaka kwa kuwa amewahi kufanya naye
kazi wakiwa Gor Mahia ambako alicheza baada ya kutoka kwa mkopo KCB.
Simba ilikuwa imempa nafasi
Kiongera ambaye sasa yuko kwenye kambi ya Harambee Stars inayojiandaa na
michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.
Taarifa zimeeleza Simba
inaendelea na kusaka wachezaji nchini Nigeria ili kuziba bafasi hiyo aliyokuwa
apewe Kiongera anayesifika kwa mashuti makali na mipira ya vichwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment