OKWI |
Uongozi wa Yanga, umesema
Agosti 17 ndiyo siku rasmi utakaotangaza wachezaji inaowaacha.
Hadi sasa gumzo katika
wachezaji watakaoachwa ni washambuliaji Waganda, Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza.
Kiiza na Okwi wanalazimika
kugombea nafasi moja iliyobaki ya wachezaji wa kigeni.
Yanga imekuwa ikiendelea
kujadili mfululizo kuhusiana na nani ataachwa kati ya hao wawili.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema Agosti 17, lazima
itajulikana ni yupi atakuwa ameachwa.
"Hiyo ndiyo siku rasmi ambayo tutatangaza kikosi chetu rasmi na wachezaji walioachwa," alisema.
Hata hivyo inaonekana suala
la Okwi na Kiiza, linaweza likajulikana mapema zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment