August 3, 2014

WANACHAMA WAKIWA NA MAKABLASHA YA FEDHA ZINAHOTAKIWA NA SIMBA, MATUMIZI NA KIASI KINACHOTARAJIWA KUINGIZWA.  
Baada ya miaka minne, leo wanachama wa Simba kwa mara nyingine wamefanikiwa kupata matumizi na mapato ya klabu yao.


Katika mkutano uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi jijini Dar, wanachama hao walishirikishwa jambo hilo la mapato na matumizi.
Wanachama hao wa Simba, tena kwa nafasi leo wamepewa karibu kila mmoja ripoti hiyo na kujua klabu yao ina mpango wa kuingiza kiasi gani na inahitaji kiasi gani.

Hivyo wana nafasi ya kuhifadhi kumbukumbu ambayo itawawezesha kuhoji lolote litakaloenda kombo.
Kwa miaka yote minne ya uongozi wa Ismail Aden Rage, hawakuwa wakihusishwa kwenye ripoti za mapato na kwenye mikutano zilikuwa zikipelekwa harakaharaka.
Uongozi wa Rage ulitumia ukali na mara nyingi wanachama hawakuhusishwa hata kidogo katika suala la fedha.

MJUMBE SURU AKIZUNGUMZA

RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA AKIZUNGUMZA




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic