August 7, 2014



Kwa kuwa amejua Real Madrid sasa haimhitaji baada ya kupata kipa mwingine mpya, Diego Lopez ameanza juhudi za kutafuta sehemu ya kwenda.

Ingawa kumekuwa na taarifa anataka kwenda Monaco ya Ufaransa, lakini sasa inaonekana atakwenda AC Milan ya Italia kwa mkopo.
Hali hiyo inatokana na Madrid kumnasa Keylor Navas aliyeng'ara kwenye Kombe la Dunia akiwa na Costa Rica na sasa atasaidiana na mkongwe Iker Casillas.

Imeelezwa AC Milan maarufu kama 'Rossoneri' inaonekana kuvutiwa naye na kocha wake, Filippo Inzaghi, ndiye anayevutiwa zaidi na kipa huyo.
Tayari Inzaghi amemueleza meneja mkuu wa AC Milan, Adriano Galliani kuhakikisha anampata kipa huyo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic