Rais wa Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu
wake mwandamizi Julio Grondora.
Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa
miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa
Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).
Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi
mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu,
na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati
wote.
Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa
miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA
na familia nzima ya Fifa na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu cha msiba huo mzito.
0 COMMENTS:
Post a Comment