August 1, 2014



Martin Odegaard ni dogo wa miaka 15 tu ambaye anacheza timu ya Ligi Kuu nchini Norway ya Stromsgodset.

Ameanza kucheza soka la kulipwa Mei, mwaka huu lakini tayari Real Madrid iko tayari kumwaga pauni milioni 12 kumpata.
Usajili ambao unaonekana ni ghali kwa umri wake. Tayari Manchester United na Bayern Munich, pia zimewahi kutupa macho kwa kijana huyo.
Halafu magwiji hao wakatoa mwaliko na kijana huyo akafanya mazoezi Munich na Manchester, hivyo nao wako mbioni.
Timu takribani 20 sehemu mbalimbali Ulaya zinamhitaji mchezaji huyo, kwa hali na mali. Jiulize ana uwezo gani, maana tayari ameishapiga mabao matatu katika ligi kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic