Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,
Zacharia Hans Poppe amesema walichokifanya Yanga, ndicho kinachowarudia.
Hans Poppe amerusha dongo nilo Jangwani
ikiwa ni kuonyesha kwamba Yanga walimsajili Okwi wakati Simba ikiwa inaidai
Etoile du Sahel dola 300,000.
“Lazima wajue unapomtendea mwenzako, kesho
yake kinarudi kwako,” alisema Hans Poppe ambaye ndiye injini ya usajili ya
Simba.
Awali Hans Poppe alieleza kuwa Okwi ameomba
kurudi Simba na wao wamempokea kwa mikono miwili.
“Tumempokea baada kuipokea barua yake na kuijadili, kwa kuwa
Yanga wamemuacha na hata FIfa inasisitiza wachezaji kupata nafasi ya kucheza
ili kuepusha kuua vipaji vyao, tumeamua kuwa naye,” alisema Hans Poppe.
0 COMMENTS:
Post a Comment