August 7, 2014


Hii ilikuwa ni mechi ya waliooa na wasiooa, kwa waandishi wa habari. Hapa ‘bachela’, Saleh Ally anapambana na aliyeoa, Ally Mkongwe katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Mechi ilimalizika kwa ‘mabachela’ kushinda kwa mabao 2-1, bao moja likiwa limepachikwa kimiani na Saleh Ally ambaye alimtoka Mkongwe na mabeki wengine wawili.
Nyuma; wanaonekana ni Wilbert Molandi na Sweetbert Lukonge wa timu ya 'mabachela' ambao hadi sasa bado ni 'mabachela' si kama mwenzao Saleh Ally.
Aidha, Saleh Ally alizawadiwa mchezaji bora wa mchezo, tuzo aliyokabidhiwa na Rais wa TFF, Leodeger Tenga wakati huo akiwa katika mhula wake wa kwanza wa uongoz. Kweli siku hazingandi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic