August 7, 2014



Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ameamua sasa kikosi chake kitafanya mazoezi asubuhi na tayari kimeingia kambini jijini Dar es Salaam.

Uamuzi huo wa Loga unatokana na mechi ya kirafiki dhidi ya Zesco ya Zambia, keshokutwa Jumamosi, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Simba imeendelea na mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Veteran nje kidogo ya jiji ili kujiweka sawa zaidi.
Awali Simba walikuwa wakifanya mazoezi jioni tu ili kupasha moto kabla ya kuanza safari ya kuweka kambi mjini Zanzibar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic