August 6, 2014

MAGULI


Simba sasa imekuwa imekuwa timu yenye ushindani mkubwa katika safu ya ushambuliaji.
Kocha Zdravko Logarusic ndiye atakuwa mwenye uamuzi wa mwisho lakini uwezo ambao ameanza kuuonyesha Elias Maguri, tayari unazidisha ushindani huo.
Kutua kwa Maguli klabuni hapo aliyetokea Ruvu Shooting kunaonekana kuwa na changamoto kubwa pia kwa straika Mrundi Amissi Tambwe, kutokana na uwezo wake wa kutupia mabao yanayomkuna Loga wanapokuwa mazoezini.
Simba kwa sasa inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Ununio, Boko nje kidogo ya Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Zesco ya Zambia unaotarajiwa kupigwa Agosti 9, mwaka huu.
Katika mazoezi ya juzi Jumatatu, Maguli alionyesha kiwango kikubwa cha kupambana kutafuta bao kabla ya dakika chache baadaye kufanikiwa kufunga bao kali kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi safi iliyochongwa na Said Nassor ‘Chollo’, bao ambalo lilifurahiwa mno na wachezaji wenzake pamoja na mashabiki.
Bao la Maguli lilinogesha upinzani unaotarajiwa msimu ujao klabuni hapo baina yake na Tambwe kwani Mrundi huyo naye pia alifunga bao moja pekee na kushindwa kudhidhirisha nani mkali mazoezini hapo siku hiyo.
Pamoja na hayo, Ijumaa iliyopita ambayo ilikuwa siku ya kwanza kwa Maguli kuanza mazoezi na Simba, alifanikiwa kufunga mabao mawili makali yaliyoonekana dhahiri kumkuna Loga baada ya kocha huyo kutabasamu kufuatia bao la pili la mshambuliaji huyo.

Hali halisi inaonekana mazoezini kwa Simba kuwa kutakuwa na vita kubwa sana kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic