Kocha wa Taifa
Stars, Mart Nooij amesema ana imani kubwa na kikosi chake kilicho hapa MSumbuji
na watafanya kila linalowezekana kupata bao la mapema.
Nooij aliyewahi
kufanya kazi nchini hapa, atakuwa na kazi ngumu leo dhidi ya Msumbiji katika
mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika raundi ya pili ya michuano ya
Afrika.
Mechi hiyo ndiyo
itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia hatua ya
makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali
itakayofanyika mwakani nchini Morocco.
Katika mechi ya
kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu hizo
zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi lenye
timu za Cape Verde, Niger na Zambia.
Akizungumza hapa
Maputo, Nooij amesema anaamini kikosi chake kitacheza vizuri zaidi kuliko
kilivyofanya jijini Dar es Salaam kwa vile hakitakuwa katika shinikizo la
washabiki ambalo mara nyingi hufanya wachezaji wasijiamini.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia katika hoteli ya Pestana
Rovuma ikitokea Johannesburg, Afrika Kusini ambapo ilifanya maandalizi yake
mwisho, na itafanya mazoezi leo (Agosti 2 mwaka huu) saa 9 alasiri Uwanja wa
Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi ya kesho.
Kikosi hicho cha
timu ya Taifa leo imeandaliwa chakula cha jioni na Balozi wa Tanzania hapa
Msumbiji, Shamim Nyanduga.
Wachezaji Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu nao wameungana na timu leo asubuhi hapa Maputo
wakitokea Lubumbashi katika klabu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo.
Mechi
itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Uganda wakiongozwa na Dennis Batte itaanza
saa 9 alasiri kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 10 jioni.
Wachezaji waliopo
katika kiosi cha Taifa Stars hapa Maputo ni Aggrey Morris, Aishi Manula, Amri
Kiemba, Deogratias Munishi, Erasto Nyoni, Haruna Chanongo, Himid Mao, John
Bocco, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mbwana Samata, Mwinyi Kazimoto, Mrisho
Ngasa, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Ramadhan Singano, Said Moradi, Shabani
Nditi, Shomari Kapombe, Simon Msuva na Thomas Ulimwengu.
0 COMMENTS:
Post a Comment