August 9, 2014


Kocha Msaidizi wa timu ya Zesco ya Zambia aliyejitambulisha kwa jina la Thomas amesema wanachotaka ni kuifunga Simba.

Akizungumza katika Hoteli ya Sapphire Court ya Kariakoo jijini Dar waliyofikia, alisema ushindi bila ya kujali ni mechi ya kirafiki ni jambo muhimu kwao.
"Tuanze na kuwashukuru Simba kwa kutupa hoteli nzuri yenye huduma nzuri (Sapphire). Wachezaji na viongozi wamefurahia sana hapa.
"Lakini sisi tunachotaka ni ushindi, tunataka kuwafunga kwa kuwa benchi letu la ufundi linajali rekodi zaidi.
"Kazi ya ukocha siku moja utaondoka au kufukuzwa. Sasa tunataka kujua baada ya hapo tulikuwa na rekodi ya aina ipi," alisema akionyesha kujiamini.
Simba inaivaa Zesco leo kwenye Tamasha lake kubwa la Simba Day litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic