August 7, 2014



Wanachama wa Simba tawi la Home Boys eneo la Tegete jijini Dar es Salaam wameweka rekodi mpya baada ya kuahidi kutoa tani 10 ya mifuko ya saruji.


Wanachama hao wamemuambia Rais wa Simba, Evans Aveva kwamba watatoa saruji kiwango hicho kikubwa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wao eneo la Bunju.
Aveva ameiambia SALEHJEMBE, kwamba wanachama hao wamempa furaha kubwa kuhusiana na uamuzi huo.
“Wametoa ahadi hiyo wakati wa uzinduzi wa tawi lao la Home Boys ambalo lina wanachama hai zaidi ya 56.
“Niseme ni jambo zuri na linatia moyo, wanachama wengine wa Simba wanapaswa kuiga suala hili kwa ajili ya maendeleo ya klabu yetu,” alisema Aveva ambaye ni mwanachama wa kwanza wa Simba kutumikia cheo cha Rais.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic