August 8, 2014



Daktari wa Simba, Yasin Gembe, amewakataza wachezaji wawili wa timu hiyo, beki Mganda, Joseph Owino na kiungo Twaha Ibrahimu ‘Messi’ kupiga mashuti kwa kipindi hiki.


Messi na Owino kwa sasa wanasumbuliwa na matatizo ya misuli ya paja na wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa daktari mpaka pale watakapokuwa fiti.

Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Jumanne ya wiki hii, wachezaji hao walikaa pembeni wakati wenzao walipokuwa wanapiga mashuti.

 Gembe alifunguka: “Owino na Messi wanasumbuliwa na misuli ya paja, ndiyo maana hawakujumuika na wenzao kupiga mashuti, wakifanya hivyo wataweza kujisababishia matatizo makubwa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic