August 6, 2014




Howard Webb amestaafu baada ya kufanya kazi ya uamuzi kwa miaka 25, sasa.

Sasa anachukua nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi kwa ajili ya mechi za Ligi za Kulipwa (PGMOL).
Webb amechezesha mechi zaidi ya 500 za Ligi Kuu England.
Pia ana rekodi ya kuwa mwamuzi wa kwanza kuchezesha fainali ya Kombe la Dunia na Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mwaka mmoja, hiyo ilikuwa 2010.


Moja ya majukumu ya Webb ,43, itakuwa ni kufuatilia na kuongeza kiwango cha waamuzi wa PGMOL.

Lakini sasa ataonekana zaidi kwenye vyombo vya habari katika vipindi mbalimbali hasa Sky Sports, BT na BBC kupitia kipindi cha Match of The Day ambako atakuwa akitoa ushauri kuhusiana na kuboresha viwango vya uchezeshaji kwa wamuzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic