August 9, 2014



Kikosi cha Zesco ya Zambia, kimetimiza kile walichoahidi kuifunga Simba licha ya kwamba imewapa hoteli nzuri waliyofikia ya Sapphire Court ya jijini Dar es Salaam.
Katika mechi ya Tamasha la Simba Day iliyopigwa leo kwenye UWanja wa Taifa jijini Dar, Zesco ilishinda kwa mabao 3-0.
Hadi mapumziko, wageni hao walikuwa mbele kwa bao moja, lakini wakafunga mawili katika kipindi cha pili likiwemo lile la dakika za nyongeza.
Pamoja na bao hilo, Zesco walionyesha soka la kuvutia zaidi na kusababisha mashabiki wa Yanga kuwazomea mfululizo watani wao waliokuwa wakihaha.
Kocha Zdravko Logarusic, alifanya mabadiliko takribani nane, akiwajaribu wachezaji wake wapya wakiwemo wale washambuliaji watatu kutoka Botswana, Kenya na Gambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic