September 5, 2014


Mfanyakazi wa Benki ya Posta (TPB) tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam, akimlabidhi Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kadi yake ya uanachama ya VIP iliyotengenezwa na benki hiyo.
TPB ni wadhamini wa Simba ambao wamekuwa wakitengeneza kadi za uanachama za klabu hiyo ambazo pia ninatumika kuchukulia fedha kwenye mashine za ATM (Picha: Mpigapicha Wetu).

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ leo amelamba kadi yake mpya ya uanachama iliyotengenezwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB).

Kaburu amechukua kadi yake hiyo ya VIP kwenye tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa TPB, Deo Kwiyukwa amethibisha hilo na kusema Kaburu ni kati ya wanachama wa Simba wenye kadi za VIP.

“Mambo yanakwenda vizuri na wanachama wa Simba wamekuwa wakijitokeza kwa kasi.
“Tunawaomba waendelee kujitokeza kupata kadi za VIP na zile za kawaida.
“Benki ya Posta inawajali sana na kuwaunga mkono ndiyo maana tuko bega kwa bega,” alisema Kwiyukwa ambaye ni mtaalamu wa mambo ya masoko.

TPB ambayo ina matawi nchini kote ni kati ya wadhamini wa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic