September 5, 2014


Umekuwa ukiwaona wanasoka wengi wakiwa na michoro katika miili yao maarufu kama tatuu.


Sasa mshambuliaji nyota wa TP Mazembe ya DR Congo, Mtanzania, Mbwana Samatta pia amejitupia tatuu zenye lugha ya Kichina na michoro mbalimbali ambazo bado haijafahamika maana yake hasa ni nini.
Mshambuliaji huyo nyota pia wa timu ya taifa, Taifa Stars  amebadili kimuonekano kutokana na tatuu hizo.

Samatta ambaye alikuwa nchini kwa ajili ya kambi ya Stars ambapo timu hiyo imeondoka alfajiri ya leo kwenda kucheza na Burundi katika mechi ya kirafiki, alionekana akiwa na tatuu tofauti na alivyokuja nchini mara ya mwisho wakati Stars ikicheza dhidi ya Msumbiji.

Kuhusu tatuu hizo, Samatta aliliambia gazeti hili kuwa, tatuu hizo ni za muda na atazitoa baada ya mwezi.

“Hizi tatuu zinafutika baada ya mwezi, siwezi kuweka za kudumu kwa sababu mimi ni mtoto wa Kiislamu na dini hainiruhusu, tatuu zenyewe hazina maana yoyote,” alisema Samatta.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic