September 25, 2014

SIKU MWOMBEKI ALIPOONDOKA JIJINI DAR KWENDA MUSCAT, OMAN.

Kiungo wa zamani wa Yanga, Athumani Iddi Chuji na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Betram Mwombeki wamefeli majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Oman.

Wawili hao pamoja na kiungo wa zamani wa Simba, Jerry Santo wote wamefeli kuichezea timu ya Oman Club iliyo daraja la kwanza.

Baada ya majaribio ya wiki moja na mechi mbili za kirafiki, watatu hao wameonekana hawana makali ya kuisadia timu hiyo ya daraja la pili kurejea Ligi Kuu Bara.
Habari za uhakika zinaeleza Chuji na Mwombeki wanatarajia kutua jijini Dar mchana huu, wakati Santo atatua kwao Nairobi, Kenya leo jioni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic