CHIPPO |
Kocha Mkuu wa Coastal
Union, Yusuf Chippo amesema kikosi chake kipo tayari kupambana mjini Mbeya na
kinataka kurejea Tanga na pointi zote tatu.
Chippo raia wa Kenya
amesema kikosi chake kinataka kurejea na pointi tatu katika mechi yao ya pili
ambayo watacheza mjini Mbeya.
“Tuko njiani, tunatarajia
kuwasili Mbeya hivi karibuni. Tumeamua kwenda mapema na hii ni mipango ya timu,”
alisema Chippo.
Alipoulizwa hana hofu ya
kupoteza pointi zote tatu kwa kuwa Mbeya City hawatataka kufanya mchezo baada
ya mechi ya kwanza kubanwa kwa sare ya bila mabao na JKT Ruvu, akasema.
“Hatuna majeruhi, hatuna
tatizo lolote na tuko tayari kwa vita. Hatutajali wao wanawaza nini lakini sisi
ni kupambana na kujituma, tunachotaka ni kushinda.”
Coastal Union ilianza ligi
hiyo kwa sare ya ugenini dhidi ya Simba ikisawazisha mabao mawili katika
kipindi cha pili baada ya wenyeji wao kuongoza kwenye Uwanja wa Taifa kwa mabao
mawili hadi mapumziko.
0 COMMENTS:
Post a Comment