Kiungo nyota wa Yanga,
Andrey Coutinho amerejea katika kiwango chake safi kabisa na sasa ataanza
kuichezea Yanga dhidi ya Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili.
Coutinho aliikosa mechi ya
ufunguzi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro, Jumamosi ijayo
kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini tayari raia huyo wa
Brazil sasa yuko fiti baada ya kucheza mechi mazoezi leo.
“Kweli Coutinho sasa
amerejea vizuri na suala la kumtumia linabaki kwa mwalimu mwenyewe.
“Unajua kawaida, uongozi wa
Yanga hautaki kuingilia masuala ya mwalimu lakini Coutinho amepona,” alisema
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu.
Mashabiki wa Yanga walikuwa
na hamu kubwa kumuona kiungo huyo mwenye kasi na chenga za maudhi akiichezea
timu yao kwa mara ya kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment