Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ni
kati ya wadau wa soka waliojiotokeza leo kuwashuhudia Yanga wakicheza mechi yao
ya kwanza ya kirafiki ya kimataifa.
Yanga imefanikiwa kuwashinda Thika ya Kenya kwa bao 1-0
lililofungwa na mshambuliaji wake Mbrazil, Genilson Santana maarufu kama Jaja.
Hans
Poppe tayari aliwaona wakicheza Zanzibar, lakini huenda aliona ni vema kuwaona
Yanga pamoja na Jaja na Coutinho kwa ujumla kama wanaweza kimataifa.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment