September 27, 2014



Nahodha wa Man Unite ameiongoza timu yake kupungunza presha kwa kufunga bao moja kati ya mawili yaliyoiwezesha kushinda 2-1 dhidi ya West Ham United.

Lakini akaiongezea presha baada ya kulambwa kadi nyekundu pia.
Bao jingine la Man United limefungwa na Robbin van Persie.
Mshambuliaji Angel di Maria ndiye alionekana moto kwa safu ya ulinzi ya West ham.

Hata hivyo dakika tano za mwisho, Man United wakiwa pungufu walikiona cha moto baada ya kushambuliwa mfululizo na wapinzani wao waliokuwa wanataka bao la kusawazisha.

Chelsea:

Kwa upande wa Chelsea yenyewe ilifanikiwa kuitwanga Aston Villa kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Oscar, Diego Costa na William.

Man City:
Manchester City nao wakiwa ugenini dhidi ya Hull City wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 huku Frank Lampard ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Sergio Aguero akiibuka shujaa kwa kufunga bao la nne.
Bao hilo la nne ambalo liliihakikishia Chelsea ushindi, ni la nne kwake ndani ya wiki moja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic