September 21, 2014



Udhamini wa kampuni maarufu ya kuuza matairi, lim na betri za magari ya Bin Slum, imewapa neema mpya Stand United.

Stand United sasa imepata udhamini kutoka kwa benki ya Exim tawi la mkoa wa Shinyanga.

Ingawa haikuwekwa wazi, benki hiyo itatoa kiasi cha fedha na kutengeneza vifaa vya michezo.
Exim imeingia baada ya kampuni ya Bin slum kuidhamini timu hiyo kupitia matairi yake ya Double Star.
Hali hiyo imewaamsha baadhi ya wadhamini na kuamua kuingia kuidhamini kwa ajili ya Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo ikiwa nyumbani imeanza kwa kipigo cha mabao 4-1, hivyo itakuwa changamoto kwake kujitahidi ili kuwainua wadhamini na mashabiki wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic