September 20, 2014


Maafande wa JKT Ruvu wameonyesha kweli walipania kuanza ligi kwa kishindo baada ya kuishika nyumbani Mbeya City.

Katika mechi hiyo iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine, kila timu upande ulionyesha soka la kuvutia, lakini mwisho hakuna aliyeona nyavu za mwenzake.
Kipindi cha kwanza kilikuwa na mashambulizi ya zamu lakini kipindi cha pili, Mbeya City wakabadilika na kuanza kushambulia sana.
Wachezaji wake, Deus Kaseke, Mwagane Yeya na Themi Felix walionekana kupania kushinda lakini  mambo yalikuwa magumu.
Kiungo Jabir Aziz alionyesha kuwapa wakati mgumu Mbeya City akishirikiana na washambuliaji Realiants Lusajo na Iddi Mbaga.

Hadi mwisho, Mbeya City ambao walishika nafasi ya kwanza msimu uliopita, walikuwa hawajapata kitu na wageni wao hali kadhalika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic