September 26, 2014

 Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, David N'Gog ametoweka kwenye klabu yake Reims ya Ufaransa na hajulikani alipo.


N’Gog aliwahi kucheza Ligi Kuu England akiwa na timu za Bolton, Liverpool na baadaye akajiunga na Reims ya kwao Ufaransa.
Kwa mujibu wa gazeti kubwa la michezo kuliko yote duniani la L'Equipe, kumekuwa na taarifa za kuhangaika kujua aliko.
Daktari wa Reims, amesema N'Gog ,25, alikuwa mgonjwa baada ya kumtembelea hotelini.
Lakini aliporudi mara nyingine hakumkuta na vitu vyake vyote havikuwemo chumbani.
Lakini Meneja wa Reims, Jean-Luc Vasseur amesema anaamini N'Gog atakuwa yuko jijini Paris alipokwenda kuitembelea familia yake.
Mwaka 2008, N'Gog alijiunga na Liverpool akitokea PSG. Alifanikiwa kufunga mabao 9 katika mechi 63 alizocheza.
Baadaye akatua Bolton mwaka 2011, akacheza mechi 81 na kufunga mabao 14.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic