Ile mechi ya Yanga dhidi ya Simba imesogezwa mbele na TFF haijasema itakuwa siku gani.
Badala yake siku hiyo kutakuwa na mechi ya Taifa Stars.
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mechi
hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili
ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya
mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini, ambapo timu hiyo inatarajiwa
kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Oktoba 10 mwaka
huu ikiwa na msafara wa watu 28.
Pambano
la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi
wa dini ya Kikristo na Kiislamu.
Wakati
huo huo, kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inafanyiwa
marekebisho madogo, na marekebisho hayo yatatangazwa kesho (Septemba 26 mwaka huu).
0 COMMENTS:
Post a Comment