CHOVE |
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
limetangaza kumzuia kipa Jackson Chove kuendelea kuicheze JKT Ruvu kutokana na
matatizo aliyoyapata.
Chove aliumia na kuzimia kwa takribani
dakika 15 katika mechi ya kwanza kati ya JKT Ruvu ilipokuwa ikiivaa Mbeya City
mjini Mbeya.
Katika mechi hiyo ya ufunguzi wa Ligi Kuu
Bara, timu hizo zilimaliza kwa sare ya bila kufunga.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema hadi
Chove atakapowasilisha vipimo vyake kwa shirikisho hilo nalo kuviwasilisha kwa
wataalamu ili kujiridhisha kama yuko sawa.
“Kitendo cha mtu kuzimia kwa dakika 15 si
kidogo, tungependa kuhijirisha.
“Lakini tunawashauri wenzetu wa klabu
kuhakikisha wanalizingatia suala la kuwapima wachezaji wao kwa kuwa mchezo wa
soka si kitu lahisi,” alisema Malinzi.
Timu nyingi za Ligi Kuu Bara na hata ligi
nyingine, zimekuwa hazifanyi vipimo vya uhakika kwa wachezaji wake kabla ya
kuanza kwa ligi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment