Mke wa beki wa zamani wa Simba, Victor Costa Nampoka amelia na kusema umasikini unaendelea kuwamaliza hasa baada ya nyumba yao kuteketea na moto.
Jasmin
Badar ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, amesema anaona
anatumbukia tena kwenye vita ya kujikomboa baada ya nyumba hiyo eneo la Tegeta
jijini Dar es Salaam kuteketea.
“Umasikini
huu jamani, kama unavyoiona, nyumba yote imeteketea, kweli inatia uchungu sana,”
alisema Jasmini ambaye alishinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa Simba.
Masaibu hayo yameikuta familia ya Costa wakati akiwa mkoani Shinyanga na timu yake ya sasa ya Mwadui FC.
Costa amesema chanzo cha moto huo ni kibatari kilichowashwa baada ya umeme kukatika na baadaye moto wa kibatari kushika kwenye pazia na kwa kuwa watu hawakuwepo ndani, moto ule ulisambaa.
Costa aliongeza kuwa moto huo umeteketeza kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba na hakuna kilichosalimika.










0 COMMENTS:
Post a Comment