Klabu ya Azam FC, imekuwa kinara wa
kuwa na wachezaji wengi kwenye timu ya taifa, Taifa Stars, baada ya wachezaji
wake kumi kuitwa kwenye timu hiyo.
Stars inajiandaa na mchezo wa kirafiki
dhidi ya Benin utakaopigwa Oktoba 12 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Wachezaji ambao wameitwa katika kikosi
cha timu ya taifa kutoka katika klabu hiyo ni pamoja na mabeki Said Moradi,
Aggrey Morris, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Gadiel Michael, viungo ni Salum
Abubakar ‘Sureboy’ Himid Mao na Mcha Khamis na makipa Mwadini Ali na Aishi Manula.
Wachezaji kutoka Yanga ni saba na
Simba ni wanne pekee na mmoja kutoka Mbeya City pamoja na wale wanne ambao wanacheza nje ya
nchi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa
Habari wa Azam, Jaffar Idd, alisema kuwepo kwa wachezaji 10 katika timu ya taifa
ni wazi kuwa kikosi chao ni bora
na hicho kinazidi kuwapa matumaini ya kuendelea kupigana.







0 COMMENTS:
Post a Comment