![]() |
| STAND UNITED, IMEPANDA MSIMU HUU. |
Timu nne zinatarajiwa kupanda Ligi Kuu
Tanzani Bara msimu ujao huku timu mbili pekee msimu huu zikishuka daraja ili kuweza
kuandaa mpango mpya wa msimu wa mwaka 2015/2016, ambapo timu 16 ndizo
zitakazoshiriki ligi hiyo.
Kwa sasa ligi kuu ina timu 14 pekee, ambazo zinashiriki na
kila msimu zilikuwa zikishuka timu tatu pekee na kupanda tatu kutoka daraja la
kwanza.
Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas
Mwakibinga, amesema kuwa msimu ujao ni timu nne kutoka daraja la kwanza ndizo
zitakazopanda na msimu huu mbili zitashuka.
Mwakibinga alisema mpango huo utaanza
msimu ujao na kwa sasa waliopo daraja la kwanza wanatakiwa kuonyesha bidii kwa
kiasi kikubwa kuhakikisha wanafanikiwa kupanda.
“Timu nne msimu ujao ndizo
zitakazopanda ligi kuu na mbili msimu huu ndizo zitakazoshuka, bidii na uwezo
wako wa kupata pointi kihalali ndiyo vitakufanya kutoka chini kuja juu na wengi
itawabidi warudi huku chini na kujipanga upya,” alisema Mwakibinga.








0 COMMENTS:
Post a Comment