Kamati
ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia wakili Damas Ndumbaro
kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha fedha.
Ndumbaro
ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wiki
iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato
yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini
wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam TV.
Ndumbaro
alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza
kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku
akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro
alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano
mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa shirikisho, Malinzi.
Kikao
cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na
kumlilipisha faini kwa sababu, Ndumbaro ambaye alizungumza kama wakili wa klabu
za ligi kuu kupitia,.
TFF imedai Ndumbaro amekanwa na klabu ingawa taarifa zinaeleza si kweli kwa kuwa viongozi wa klabu 12 walisaini kumpitisha kuwa wakili wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment