October 8, 2014


Siku moja baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumshitaki mwanasheria Dk Damas Ndumbaro kwenye kamati ya nidhamu, yeye ameibuka na kusema anaona kilichofanywa na shirikisho hilo ni maajabu ya karne.

Dk Ndumbaro amesema anaona ni maajabu kwake kushitakiwa kwa ajili ya kuwatetea wateja wake ambao ni klabu za Ligi Kuu Bara.
“Sijawahi kusikia wala haijawahi kutokea kusikia mwanasheria anashitakiwa kwa ajili ya kuwatetea wateja wake.
“Mimi ni mwanasheria nah ii ndiyo kazi yangu, sasa nashangazwa kushitakiwa kwa ajili ya kuwatetea wateja wangu, hiki ni kitu cha ajabu kabisa.
“Lakini nimeaandikia barua TFF kuwaeleza sitaweza kuhudhuria kikao hicho cha kamati ya nidhamu kesho kwa kuwa ninaondoka kwenda nchini Marekani kutokana na mwaliko wa chuo kikuu kimoja huko.
“Nitakuwa nikitoa mafunzo kwa siku Oktoba yote, lakini bado ninataka kujua ninashitakiwa kwa ajili ya nini na nani,” alisema Dk Ndumbaro akionyesha kujiamini katika hilo.
“Katika barua niliyopewa na TFF haielezi nani anayenishitaki, pia haielezi kosa langu zaidi ya kusema mambo niliyoyazungumza. Yapi.”
Dk Ndumbaro ndiye mwanasheria anayezitetea klabu za Ligi Kuu Bara ili kuepuka TFF kuzikata asilimia 5 kwenye udhamini wa Vodacom na Azam TV.

Pia, Serikali imeishaagiza suala hilo kusitishwa hadi hapo bodi ya ligi na TFF zitakapokutana Jumamosi na kujadiliana, zifikie mwafaka halafu zirudi serikalini.

2 COMMENTS:

  1. Ndumbaro anawatetea nani wakati Simba na Yanga zimekana kumtambua?Acha uzushi wewe Saleh!

    ReplyDelete
  2. TFF inaleta ukoloni wakati nchi imeshapata uhuru, haiwezekani taasisi ikatoa maamuzi yanayowaathiri wadau wake kwa namna yoyote ile bila kuwahusisha, tena bila haki ya wao kuhoji..! huo ni upuuzi usiovumulika wala kukubalika...!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic