October 7, 2014

Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane ametoa kali baada ya kueleza kuwa Real Madrid waliwahi kumpigia simu wakitaka ajiunge nao wakati akiwa msalani.

Lakini kutokana na uoga, aliamua kuikata kutokana namba kutoonyesha jina la aliyepiga.
Mkurugenzi wa Michezo wa Real Madrid wakati huo, Emilio Butragueno ndiye aliyempigia kiungo huyo wa Man United wakati huo.
Ilikuwa ni mwaka 2005 wakati akiwa mbioni kuachana na Manchester United na mwisho akaamua kwenda Celtic.
Wakati anapigiwa, wakati huo wakala wake Michael Kennedy alikuwa katika hatua za mwisho kumfanyia mpango huo wa kujiunga na Celtic ya Scotland.
Yote hayo, Keane ameyaelezea katika kitabu chake kipya cha maisha yake kikiwa ni cha pili na amekipa jina la Second Half, yaani kipindi cha pili.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic