Kipa Iker Casillas amesema anawaelewa mashabiki kama binadamu hata inapofikia sehemu wanamzomea.
Amesema amekuwa akiumia kutokana na wanavyomzomea, lakini anaamini kama bindamu wanaweza kuwa wamechoshwa na uso wake.
"Wakati mwingine watu wanahitaji vitu, kiwango changu hakijashuka lakini huenda wanataka kuona kitu kingine.
"Yaani sura mpya hapa langoni, ni suala la muda. Ikifika siku sitakuwa na ujanja, ila kwa wakati huu wanapaswa kuniunga mkono," alisema.
Casillas amesema ulifikia wakati alikuwa akifikiria kuondoka Real Madrid kwa kuwa aliona hakuwa akitendewa haki.
Lakini uvumilivu na maneno ya kiungwana ya waliomzunguka yalimsaidia.
KUHUSU JOSE MOURINHO:
Kipa Iker Casillas amesema
aliamua kukaa kimya, kutojibizana na aliyekuwa kocha wake, Jose Mourinho sababu
ya kulinda maslahi ya Real Madrid.
Akijibu swali aliloulizwa
na mwandishi IƱaki Gabilondo katika mahojiano maalum, Casillas alisema haikuwa
sahihi kuzozana na Mourinho huku akijua inayoathirika zaidi ni Madrid.
“Ningeweza kumjibu
Mourinho, nilinyamaza kwa manufaa ya klabu. Sikuona kama ni sahihi kuwasha moto
ambao ungeuunguza klabu.
“Hatukuwa tukizungumza
vizuri hata kwenye mikutano ya waandishi tulienda wote, lakini hatukuzungumza.
“Mwanzo sikujua kama
walikuwa na matatizo na mimi, lakini nilipoumia ndiyo nikagundua kuna kitu.
“Kwani hata baada ya
kurudi kutoka majeruhi, kila siku msaidizi wake aliendelea kusema sikuwa fiti
na mashindano.








0 COMMENTS:
Post a Comment