October 14, 2014


Kipa wa zamani wa kimataifa wa Bosnia, ametoa kali baada ya kumtwanga mwamuzi konde kali.

Romeo Mitrovic, alimpiga mwamuzi konde katika mechi ya daraja la pili, baada ya kulambwa kadi ya njano.

Kipa huyo aliyewahi kuichezea timu yake ya taifa mwaka 2006 ilipochapwa mabao 2-0 dhidi ya Korea Kusini, alionyesha kukerwa na kadi hiyo, hivyo kuchukua uamuzi huo mkali.

Alionyesha kadi baada ya kupoteza muda, ilionekana kipa huyo wa HNK Branitelj kama alifanya mzaha.

Haraka akamkimbilia mwamuzi na kumchapa konde, mwamuzi akatimua mbio kuomba msaada wa askati ambao walimzunguka wakati akimpa kipa huyo kadi nyekundu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic