Kocha maarufu barani Ulaya,
Roberto Mancini ameibuka na kusema anaamini Liverpool ndiyo nafasi ya mwisho
kwa mshambuliaji Mario Balotelli.
Mancini aliwahi kuwa kocha
wa Balotelli wakati wote wakiitumikia Man City na walikuwa wakilumbana mara kwa
mara kocha huyo akimtuhumu Balotelli kwa utovu wa nidhamu.
Balotelli ameanza kwa
kusuasua na Liverpool akiwa amejiunga nayo kwa kitita cha pauni milioni 16
akitokea AC Milan ya Italia.
Mancini amesema Balotelli
ana nafasi ya kuonyesha alichonacho sasa.
Amesisitiza iwapo atafeli
Liverpool, basi atakuwa amejiweka katika wakati mgumu.
Hadi sasa Balotelli
amefunga bao moja tu akiwa na Liverpool, lakini Mancini amesema anaweza
akafanya vizuri zaidi kama walipokuwa pamoja Inter Milan na baadaye Manchester
City.
0 COMMENTS:
Post a Comment