October 27, 2014


Kikosi cha Simba kinaondoka mjini Mbeya na kwenda kuweka kambi mjini Iringa.
Kikosi cha Simba kinatokea mkoani Mbeya ambako kilicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara nje ya Dar na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Prisons.

Simba inakwenda kuweka kambi kwa siku mbili mkoani Iringa kabla ya kuondoka kwenda Morogoro tayari kuivaa Mtibwa Sugar.
Mtibwa Sugar pia iko Mbeya ambako ilicheza mechi dhidi ya Mbeya City na kuitungua kwa mabao 2-0.
Mtibwa imekuwa inakwenda na mwendo mzuri huku ikishinda mechi zake kwa asilimia 90.
Hali inayowalazimu Simba waliotoka sare tano katika mechi tano kutakiwa kujiandaa vilivyo.

“Kweli tutaanza safari ya kwenda Iringa ambako tutaweka kambi,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic