Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaingia kambini kesho (Oktoba 6 mwaka huu)
kujiwinda kwa mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaingia kambini kwenye hoteli ya
Accomondia jijini Dar es Salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 26 walioitwa na
Kocha Mart Nooij kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 jioni.
Kwa
mujibu wa Kocha Nooij, timu hiyo itakuwa na vipindi (sessions) 11 vya mazoezi
kabla ya kucheza na Benin (Squirrels). Stars itafanya mazoezi asubuhi na jioni
kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ambapo baadhi yatafanyika Uwanja wa Taifa, na
mengine kwenye uwanja mwingine.
Wachezaji
Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Mwinyi Kazimoto anayechezea timu ya Al
Markhiya ya Qatar wanawasili nchini kesho (Oktoba 6 mwaka huu).
Naye
mshambuliaji Juma Liuzio anayechezea timu ya Zesco ya Zambia atawasili nchini
keshokutwa (Oktoba 7 mwaka huu) kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola.
0 COMMENTS:
Post a Comment