![]() |
| MOHAMMED HUSSEIN 'SIMBA', AMEITWA PIA. |
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya maboresho ya timu ya Taifa
(Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini ya miaka miaka 23.
Katika awamu hii, Kocha wa Taifa Stars,
Mart Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao watakuwa wakiingia kambini mara
moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya kuwakilisha timu zao kwenye mechi za
ligi.
Kikosi hicho cha maboresho kitakuwa
kikifanya programu maalumu za mazoezi mpaka siku ya Jumatano na kucheza mechi
za kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.
Lengo hasa la programu hiyo ni kuwajengea
uwezo vijana wenye vipaji ambao walipatikana katika awamu ya kwanza ya mpango
wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu Tukuyu mkoani Mbeya, lakini wamekuwa
hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili kujenga timu ya ushindani na imara ya Taifa
ya muda mrefu.
TFF ina imani kubwa kuwa programu hii
itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania. Timu hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka
huu katika hoteli itakayotangazwa baadaye.
Wachezaji walioteuliwa ni Aishi manula
(Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Aboubakar Ally (Coastal Union), Miraji
Adam (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel
Semwanda (African Lyon) na Joram Mgeveke (Simba).
Edward Charles (Yanga), Hassan Mwasapili
(Mbeya City), Kassim Simbaulanga (African Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam
Salamba (Kahama), Hassan Banda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma
(Stand United), Makarani Ally (Mtibwa Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis
(Simba).
Aboubakary Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan
Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita Gold), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar),
Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda SC), Kelvin Friday (Azam),
Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Alfred Masumbakenda (Kahama) na Simon Msuva (Yanga).








0 COMMENTS:
Post a Comment